https://monetag.com/?ref_id=TTIb Wanafunzi waliochafua picha ya Rais wafukuzwa shule | Muungwana BLOG

Wanafunzi waliochafua picha ya Rais wafukuzwa shule


Wasichana watatu walioshtakiwa kwa kuharibu picha ya Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza kwenye kitabu na Wanafunzi wengine wawili wamefukuzwa shule, siku kadhaa baada ya kuachiwa kwa dhamana. Mkuu wa Shule ya l'Ecofo Akamuri amesema wamefukuzwa kwa kuharibu vitabu vya shule.

Awali wasichana hao walishikiliwa takribani majuma mawili kwa shutuma za kumtusi Rais kitu kilichopelekea kuzuka kampeni mitandaoni za kutaka wasichana hao waachiliwe huru.

Kwa mujibu wa BBC Waziri amesema wasichana hao wenye miaka 15,16 na 17 waliachiwa huru kwa muda wiki tatu zilizopita na sasa wamefukuzwa shule.