Loading...

4/23/2019

Waziri Mwakyembe awashangaa wanaomuulizia Mwandishi Azory Gwanda


Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amewashangaa watu wanaofuatilia mahali alipo mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Azori Gwanda.

Dk Mwakyembe ameyasema hayo bungeni leo alipokuwa akihitimisha mjadala wa bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2019/20.

"Tunaongelea kesi ambayo ni dhaifa sana tena sana, Eneo alilopotea Mwandishi huyu ni eneo ambalo Mamia ya Watanzania wamepotea , hawawaulizii hao huyo mmoja ndio dhahabu, alafu inaulizwa serikali ambayo imeshughulikiwa kwa kiasi kikubwa kweli kweli, Maafisa wetu wa serikali wamekufa kule," alisema Mwakyembe.

“Pamoja na hayo Serikali itaendelea kudhibiti watu wanaokiuka utoaji wa maoni kwa kuwa hakuna uhuru usiokuwa na mipaka,”amesema Dk Mwakyembe.


Loading...