https://monetag.com/?ref_id=TTIb Akaunti 'feki' Bil. 3 za Facebook zafungwa | Muungwana BLOG

Akaunti 'feki' Bil. 3 za Facebook zafungwa


Mtandao wa Facebook umechapisha orodha ya mabilioni ya akaunti feki ilizochukulia hatua kati ya mwezi Oktoba 2018 na Machi 2019.

Katika kipindi hicho cha miezi sita, Facebook ilifunga zaidi ya akaunti bilioni tatu feki - idadi ambayo inasema ni kubwa zaidi kuwahi kufungwa.

Zaidi ya ujumbe milioni saba za"chuki" pia zilitolewa katika mtandao huo wa kijami.

Kwa mara ya kwanza, Facebook pia iliripoti kuwa baadhi ya watumiaji wa mtandao huo ambao ujumbe wao ulifutwa wamekata rufaa na kuongeza kuwa zingine zilirudishwa baada ya uchunguzi wa kina.

Akizungumza na vyombo vya habari mwanzilishi wa mtandao huo, Mark Zuckerberg aliwakosoa vikali wale ambao wanatoa wito kampuni hiyo ivunjwe mbali, akiongeza kuwa wanafanya kila wawezalo kukabiliana na changamoto zinazoibuka.