Loading...

5/19/2019

Arnold Schwarzenegger apigwa teke kwenye hafla Afrika Kusini


Kanda ya video imeonyesha kuwa nyota wa filamu Hollywood Arnold Schwarzenegger akishambuliwa katika hafla moja nchini Afrika Kusini.

Gavana huyo wa zamani wa jimbo la California mwenye umri wa miaka 71 alikuwa akizungumza na mashabiki wake wakati wa mashindano ya kuruka kamba katika hafla yake ya michezo barani Afrika wakati mtu mmoja alipompiga teke kutoka nyuma.

Hata hivyo mwenyewe anasema hakuhisi kama alipigwa teke alijua ni fujo za mashabiki ila anashukuru mtu huyo hakumwaribia video yake ya snapchat
Loading...