Asilimia 85 ya wanaume na 65 ya wanawake wanatoka nje ya Ndoa


Waumini wa dini ya Kikirsto na wasio wakristo wametakiwa kuishi kwa toba na hofu ya Mungu na kuepuka dhambi ya usaliti ambayo madhara yake ni makubwa kimwili na kiroho.

Akiwahubiria waumini  katika Ibada ya jumapili  leo May 20 katika  Kanisa la Lutheran [KKKT] Usharika wa Babati mjini mtaa wa Komoto mtumishi wa Mungu Godamen Merinyo  amesema dunia ya sasa wengi mioyo yao imejaa ghadhabu kwa sababu  ya usaliti.

Mhubiri huyo amesema katika kitabu kimoja kilichoandikwa na Mtheolojia,alisema asilimia 85 ya wanaume wanaume na wanawake asilimia 65 wanatoka nje ya ndoa na yote hayo yanasababishwa na mwanamke mwenyewe.

“Sisi wanaume ni wadhaifu sana,ni sawa na mkate na chai”alisema Merinyo.

Ameendelea kusema kuwa mwanamke  ambaye ameolewa sio kwa sababu ya kufua au kumpikia mwanaume huyo aliemuoa bali  ni kwa ajili ya kufanya tendo la ndoa.

Amesema wanawake wengi wanasababisha wanaume wao kutoka nje kwa sababu ya vijitabia ambavyo vinamkera mwanaume ikiwemo Uchafu na mavazi kwa baadhi yao.

Amesema muda mwingine usaliti ni kama kumpiga chura teke kwani wapo baadhi ambao wameshafanyiwa hivyo lakini ukiwatizama leo hii wana maisha mazuri baada ya kusalitiwa na wenza ndugu zao walioaidiana mengi.

Hata hivyo amewatia Moyo waliosalitiwa kwa kuwaeleza kuwe wasife moyo kwani binadamu anaweza kukusaliti lakini Mungu kamwe hawezi kukukuacha katika hali yeyote ile.