Askofu Kakobe mbele ya Gwajima, 'Sikuja hapa kutetea uzinzi'



Askofu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe leo alifika Kanisa la Ufufuo na Uzima kwa Josephat Gwajima katika sherehe za kanisa lake kutimiza miaka 30.

Katika mazungumzo yake aligusia kile kilichotokea hivi karibuni kusambaa kwa video chafu zilizodaiwa kuwa ya Askofu Gwajima.

"Mimi sina mchezo na dhambi, sikuja hapa kutetea uzinzi, katika kanisa letu ni wakali sana kuhusiana na masuala ya uzinzi.Katika ile video yule mwanamke anayedaiwa kutembea na Gwajima sura yake haionekani, Kanisa haliwezi kutikiswa kila rahisi hivyo," ameeleza.

Alisema katika video iliyosambazwa mshtaki yupo wapi kama amejificha na hataki kuonekana kiblibilia hizo zinaitwa fitina.

Aliendelea kwa kusema, "Video fake zinatengenezwa na Leo sina sababu ya kwenda ndani ya hilo, Sasa hivi watoto wadogo wa shule wenye teknolojia wana uwezo wa kutengeneza video fake".