Chanzo kikuu cha kukatika kwa umeme chatajwa


Serikali imesema tatizo la kukatika umeme nchini linatokana na uwepo wa baadhi ya miundombinu mibovu ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ambayo haijabidilishwa tangu enzi za mkoloni hadi sasa.

Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani ameyasema hayo leo Jijini hapa wakati akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo, Tangu kuanzishwa kwa shirika hilo mwaka 1918 enzi za mkoloni, bado baadhi ya miundombinu hiyo haijabadilishwa, katika bajeti ya wizara wameomba fedha ili kukabiliana na changamoto hiyo.

“ Tumeeleza kwenye bajeti yetu, tumeomba fedha na tumepata fedha kwa ajili ya kukabiliana na changamoto hiyo kwa sababu lengo la serikali ni kutokomeza kukatika kwa umeme,” amesema Dk Kalemani.

Ametaja changamoto nyingine ni pamoja na viwango vya umeme kuwa juu, anaimani kuwa baada ya ujenzi wa miradi mbalimbali kukamilika bei hizo zitashuka.