https://monetag.com/?ref_id=TTIb DC Meru apiga marufuku Makanisa kubomolewa | Muungwana BLOG

DC Meru apiga marufuku Makanisa kubomolewa



Na Ferdinand Shayo ,Arusha.

Mkuu wa wilaya ya Meru Jerry Muro amepiga marufuku wataalamu wa halmashauri hiyo kubomoa makanisa yaliyojengwa kwenye makazi ya watu na kusababisha adha ya kelele kwa watu na badala yake ameshauri makanisa hayo yafunge vidhibiti sauti maarufu kama sound proof.

Jerry Muro amesema hayo wakati akizungumza na Viongozi wa dini na makanisa mbalimbali yaliyopo Wilaya ya Meru ambapo amewataka viongozi hao kushirikiana vyema na serikali kwani inatambua mchango wake katika maendeleo.

Askofu wa Kanisa la International Evangelism Eliud Isangya amesema kuwa Wilaya ya Meru itaweza kukua na kustawi katika Nyanja zote kwa kuwa na viongozi wenye hofu ya Mungu na wanaowajibika.

Kwa upande wao Viongozi wa Dini Sekela Rowland,Samson Tiyere,Lubunga Simu waliohudhuria katika mkutano huo wamempongeza Mkuu wa Wilaya kwa kuwashirikisha Viongozi wa dini katika masuala ya kimaendeleo na kutatua changamoto za taasisi Za dini.

Mkuu wa Wilaya ya Meru amefanya mkutano wake na Viongozi wa dini ikiwa ni pamoja na kuandaa hafla fupi ya kushiriki chakula na viongozi wa dini.