DC Muro atimiza ahadi kwa manusura wa ajali ya moto


Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Cornel Muro amekabidhi Mifuko Ishirini ya Saruji ( Cement) ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake ya kuisaidia familia ya Bw Eliud Samwel Nyari ambaye nyumba yake iliungua kwa moto na kusababisha kifo cha mtoto wake wa kike Mercy mwenye umri wa miaka miwili na nusu katika kijiji cha Loita Nkwamala kata ya Nkwandrua Halamashauri ya Meru.


Dc Muro amekabidhi mifuko hiyo 20 kwa mjumbe wa Kamati ya kusaidia kumjengea Nyumba, Ndugu Eliud ambae yeye na familia yake yenye watu saba kwa sasa hawana mahali pa kuishi uku wakiwa na majonzi ya kuondokewa na binti yao mpendwa Mercy aliefariki kwenye ajali ya moto.

Pia Dc Muro ameomba wasamaria wema kusaidia kuchangia vifaa vya ujenzi yakiwemo mabati, nondo na mchanga pamoja na cement ili kuiwezesha familia hiyo kupata sehemu ya kiwasitiri na kuendelea na maisha .