Diego Maradona akamatwa kwa kushindwa kulipa deni

Nyota wa soka  wa Argentina,Diego Maradona atiwa nguvuni nchini Argentina kwa kushindwa kulipa deni la Euro milioni 5 kutoka kwa mpenzi wake wa zamani Rocio Oliva.

Maradona alikamatwa alipotua uwanja wa ndege nchini Argentina wakati akitokea nchini Mexiko. Rocio Oliva, amefungua kesi ya madai dhidi ya Maradona.

Kesi hiyo itatajwa ifikapo Juni 13.