Loading...

5/23/2019

FIFA yasitisha mpango wa Kombe la Dunia kuwa na timu 48


Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limesitisha mpango wa kuongeza nchi zitakazoshiriki Kombe la Dunia mwaka 2022 kutoka timu 32 hadi kufikia timu 48.

Rais wa Fifa Gianni Infantino mwaka jana alisema mpango wa kuongeza timu hizo kutoka 32 hadi 48 ambao ungelianza kutekelezwa mwaka 2026 urudishwe nyuma hadi mwaka 2022.

Hata hivyo, FIFA ilitathmini uwezekano wa Qatar peke yake mashindano hayo yenye timu 48 ikaona ni mdogo na ikaamua kusitisha mpango huo kutokana na changamoto ya ukosefu wa muda wa kutosha kufanya ukaguzi.
Loading...