Loading...

5/24/2019

Jinsi ya kutambua kama mwanamke anakuchukia


Unapokuwa na mahusiano na mwanamke umpendaye kwa dhati zipo dalili za wazi ambazo mwanamke huyo atakuonesha kwamba anakuchukia, siyo mpaka akwambia kwa mdomo wake bali utaona kwa vitendo kama ifutavyo;

Hajibu jumbe zako za maaandishi 
Wanawake ni viumbe ambao wanapenda kuwasiliana. Wakitumiwa jumbe na yeyote basi kwa kawaida ni jukumu lao kuhakikisha ya kuwa wanajibu. Hii ni kawaida. Lakini ukiona kuwa hajibu texts ama jumbe zako, usimuamini akikwambia kuwa alikuwa amesahau ama alikuwa yuko busy.

Kama unaona ya kuwa hajibu texts zako hio ni ishara ya haraka kukuonyesha ya kuwa hajapendezwa na wewe. Fahamu ya kuwa wale wanawake wagumu wakiwa wamekupenda basi hawatajizuia kureply texts zako.

Yuko busy kila wakati.
Anaweza kuwa ni mkurugenzi wa kampuni flani ama labda ni meneja katika shirika tajika, lakini kila mwanamke anaweka malengo yake muhimu mbele. Ukimskia kuwa hawezi kuwa na time kwa sababu muda mwingi anakuwa busy, basi unapaswa kufahamu ya kuwa anakwambia maneno hayo kwa kuwa hataki kuspend time nyingi na wewe.

Anakuambia ubaya wake.
Mara nyingi, wanawake watakuambia ubaya wao kuwahusu. Anaweza kuambia anavuta sigara, yeye ni mlevi chakari, ama ni mvivu nk. Yaani ili mradi umuone ya kuwa ni mwanamke asiyekufaa.

Ukiona mwanamke ambaye akiwa anazungumza na wewe anakuambia maovu yake, basi anakuambia ya kuwa uachane naye na utafute mwanamke mwingine ambaye ni bora zaidi kumliko. [

Anapenda kuongea kuhusu wanawake wengine.
Kama mwanamke anakupenda, mara nyingi anataka atenshen yako yote iwe kwake. Na akiona ya kuwa unaongea kuhusu wanawake wengine basi anashikwa na wivu.

Lakini huyu mwanamke ulienae ukiona anapenda kuongea kuhusu wanawake wengine na haswa kueleza mambo yao chanya, basi uwezekano mkubwa ni kuwa anakuchukulia kama rafiki tu. Na hakuoni kama mpenzi mtarajiwa.

Anapenda kuja na mtu mwingine.
Ishara nyingine kuonyesha kuwa mwanamke hakupendi ni pale ambapo ukimuita mtoke deti badala ya kuja pekeake anakuja na marafiki zake. Wanawake hupenda kutembea na marafiki zao ili kuleta furaha kwa kila sehemu ambazo wanakuwa.

hizi ni ishara muhimu lazima uzingatie. Usijisumbue kuteseka na mwanamke asiyekupenda. Ni haki yako kujua iwapo anakupenda au la. Ishara ndizo hizo tumekupa. Ukiona iwapo mwanamke ulienaye anaonyesha baadhi ya hizi tabia tulizoziorodhesha, basi epuka na mapema.
Loading...