Kagere atoa siri Simba SC


Mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere amefunguka kuwa amefurahia kuona ameisaidia timu yake ubingwa, lakini akasisitiza hiyo ni kutokana na ushirikiano wao kama wachezaji.

“Na kwa upande wa mabao nimekuwa na juhudi ya kufunga sababu niliamua kujiwekea chalenji mimi binafsi kwa kila mchezo ambao nacheza, kuwa hapa lazima nifunge, ndiyo maana nimeweza kufunga mabao hayo,” alisema Kagere.

Kagere ametwaa ubingwa huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya kwanza akiwa na kikosi cha Simba ambacho kilimsajili mwanzoni mwa msimu huu.

Nyota huyo katika msimu wake wa kwanza kwenye ligi hadi sasa amefunga jumla ya mabao 23 akiwa amesaliwa na mechi mbili kumaliza ligi hiyo.

Kagere alisema ushirikiano kati yao ndiyo imekuwa siri kubwa ya wao kuweza kutwaa ubingwa. “Furaha yangu ilikuwa kuona tunatwaa ubingwa na hilo limeweza kutimia lakini shukurani iende kwa Mungu pamoja na wachezaji wenzangu tulivyokuwa tunashirikiana na kufika hapa.

Mshambuliaji huyu akiwa hapo na Simba amefanikiwa kufunga mabao sita kwenye michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika.