https://monetag.com/?ref_id=TTIb Kampuni ya Boeing yakiri kuwepo hitilafu kwenye 'Software' ya 737 MAX | Muungwana BLOG

Kampuni ya Boeing yakiri kuwepo hitilafu kwenye 'Software' ya 737 MAX


Kampuni ya uundaji ndege ya Boeing imekiri kuwa imelazimika kurekebisha makosa kwenye “flight simulator software” ya ndege aina ya 737 MAX baada ya ajali mbili zilizoua watu 346.

Katika taarifa yao wamesema wameongeza taarifa zaidi kwa waongoza ndege ili kuhakikisha inafaa katika hali tofauti za safari.

Licha ya kukiri huko, Boeing haikusema ni lini waligundua tatizo hilo lililosababisha ajali ya ndege ya Ethiopia mwezi Machi, 2019 na ile ya Lion Air Oktoba, 2018 na wala kusema endapo waliwajulisha waratibu.

Ndege hizo zimesitishwa matumizi duniani kote zikisubiri ruhusa kutoka Marekani na waratibu wa kimataifa kabla ya kuanza kutumika tena.