Kocha wa Sevilla abwaga manyanga

Kocha wa timu ya soka  inayoshiriki ligi kuu ya Uhispania (La Liga) Sevilla, Joaquin Caparros, ametangaza hatokuwa kiongozi wa benchi la ufundi la timu hiyo msimu ujao.

Caparros amesema ataendelea kuwapo Sevilla akiwa na majukumu mengine.

Caparros  mwenye umri wa miaka 66 amekuwa kocha wa Sevilla kwa misimu 3 tofauti, mwezi April aligundulika kuwa na ugonjwa wa kansa ya damu, Lakini alisema kwamba ugonjwa huo usingeathiri kazi zake za kitaalamu.