Mbunge ataka vivutio vya Utalii vitangazwe kama Manara anavyoitangaza Simba


Mbunge wa Mufindi Kusini Cosato Chumi (CCM), ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuvitangaza vivutio vya Utalii kama ambavyo Msemaji wa Simba Haji Manara anavyoitangaza Simba.

Chumi ametoa kauli hiyo bungeni wakati akichangia Mjadala wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa  mwaka 2019-2020.

“Katika suala la michezo kuna msemaji anaitwa Manara pia kuna Thobias Kifaru wa Mtibwa Sugar wale wanazitangaza timu zao sasa  kwanini tusihamashe watu waende katika vivutio vyetu kama ambavyo wanahamasisha wale wasemaji.”amehoji Chumi.

Aidha Chumi alisema Manara anahamasisha Simba inajaza uwanja sasa ni kwanini wizara isimtumie ili kuvitangaza vivutio vya utalii.