Mgombea Urais akosa jina lake kwenye daftari la wapiga kura


Makamu wa Rais wa Malawi, Saulos Chilima, ambaye ni miongoni mwa wagombea wa urais dhidi ya Rais Peter Mutharika katika uchaguzi wa leo, amekutaa jina lake haliko katika daftari la usajili wa wapiga kura katika kituo alichojiandikisha.

Chilima, ambaye alikwenda katika kituo hicho katikati mwa mji mkuu wa Malawi, Lilongwe, asubuhi ya leo aliambiwa na wafanyakazi wa uchaguzi kusimama kando kwa kuwa jina lake halikuwepo katika daftari.

Taarifa iliyotolewa na Tume ya Uchaguzi ya Malawi (MEC) baadaye ilithibitisha tukio hilo, akisema jina la Chilima haliko kwenye daftari licha ya kuwa ameandikisha hapo.

Hata hivyo baaadaye Chilima baadaye aliruhusiwa kupiga kura kwa kuwa kulikuwa na ushahidi wa kutosha kwamba alijiandikisha katika kituo hicho, taarifa hiyo imesema.