Loading...

5/17/2019

Mkude awashusha presha mashabiki wa Simba SC


Mchezaji wa kikosi cha Simba SC, Jonas Mkude ameeleza kuwa mashabiki wa Simba wasiwe na presha juu ya kusepa kwake ndani ya Simba muda huu, bado ni mali ya Simba wakati wa Mungu ukifika ataondoka.

Mkude amesema kuwa amekuwa akisikia taarifa kwamba anaondoka Simba, jambo hilo kwa sasa halipo kwani bado anaitumikia timu yake.

"Unajua mimi ni mchezaji na mpira ndiyo kazi yangu, kuhusu kujiunga na timu nyingine kwa sasa hilo halipo, ila wakati ukifika sitawaficha ntawaweka wazi.

"Kwa sasa ambacho ninaweza kuwaambia mashabiki wa Simba ni kwamba waendelee kutupa sapoti kwenye michezo yetu iliyobaki kwani kazi bado ni ngumu na ushindani ni mkubwa na sapoti yao ni muhimu," amesema Mkude.

Loading...