Loading...

5/23/2019

Msemaji wa waasi akiri mashtaka ya ugaidi Rwanda


Nsabimana Callixte maarufu Sankara aliyekuwa msemaji wa kundi la waasi la National Liberation Front amefikishwa mbele ya Mahakama mjini Kigali na kukiri mashtaka dhidi yake.

Mwendesha mashtaka amesoma mashtaka 16 dhidi ya mshtakiwa huyo ambayo yana uhusiano na ugaidi, ujambazi wa kutumia silaha na ushirikiano na nchi ya kigeni kwa lengo la kuishambulia Rwanda.

Sankara amekiri kushirikiana na Burundi pamoja na Uganda katika kuishambulia Rwanda na ameomba msamaha kwa Serikali pamoja na familia zote zilizoathirika kutokana na uhalifu alioufanya.
Loading...