https://monetag.com/?ref_id=TTIb Mtoto mwenye ulemavu aokotwa na Wananchi | Muungwana BLOG

Mtoto mwenye ulemavu aokotwa na Wananchi


Wananchi wa Kata ya Bupingu wamemuokota mtoto mwenye ulemavu wa mkono pamoja na tatizo la akili anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 14. Mtoto huyo aliokotwa kwenye pori lililopo kijiji cha Bupingu mpaka sasa anatibiwa na kutunzwa kwenye hospitali ya Wilaya ya Ileje.
.
Mganga Mkuu Wilayani humo, Enock Mwambalaswa amekiri kupokelewa kwa mtoto huyo. Amesema mtoto huyo ambaye anaongea Lugha ya Kisafwa tu, amekuwa akiwasiliana na muuguzi(Ericka Mtali) kwenye hospitali hiyo na ikitokea muuguzi huyo hayupo inakuwa shida kwa mtoto huyo kufanya mawasiliano na wauguzi wengine.

Tabitha Swila, Afisa Ustawi wa Jamii Wilayani humo amesema, baadhi ya wazazi au walezi wamekuwa na uelewa duni kuhusu malezi kwa watoto wenye ulemavu hivyo ofisi yake imejipanga kuhakikisha inatoa elimu kwa Umma ili kuepuka hali hiyo.

Kwa siku za hivi karibu idadi ya watoto wenye ulemavu waliotupwa na kuhifadhiwa hospitalini hapo imefikia watoto 6.