Picha: Waziri Lugola awatuliza madereva waliotaka kugoma


 Waziri Lugola amewatuliza madereva wa vyombo vya moto waliotaka kugoma kutokana na kutopewa mikataba ya kazi, matumizi mabaya ya tochi pamoja na ulipaji wa faini na kusimamishwa hovyo na matrafiki mabarabarani. Lugola amewataka wamiliki wa vyombo vya moto nchini kutoa mikataba ya kazi kwa madereva na wafanyakazi mbalimbali katika makampuni yao.