Rais Magufuli atoa eneo kwa taasisi ya Al Hikma kujenga kituo cha afya


Rais Dkt Johh Pombe Magufuli amemuagiza Waziri wa TAMISEMI kuhakikisha taasisi ya Al Hikma inapewa eneo kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya huko Temeke kama walivyoomba.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mkurugenzi wa Al Hikma, Sheikh Nurdin Kishk kumueleza Rais kwamba wameomba eneo hilo siku nyingi lakini hawaelewi kwa nini hawapewa hadi sasa licha ya kupata kibali katika ngazi mbalimbali za Serikali.