https://monetag.com/?ref_id=TTIb Sababu za wanaume wengi kukimbiwa na wanawake | Muungwana BLOG

Sababu za wanaume wengi kukimbiwa na wanawake


Imezoeleka katika jamii kwamba wanaume hukimbiwa na wanawake kwa kukosa kipato au alichonacho ni kidogo, au muonekano na maumbile ya mwanaume bila kuzingatia kwamba wanawake huangalia vitu vingine zaidi ili kugundua kama wanaweza kuishi na aina hiyo ya mwanaume.

Zifuatazo ni sababu  zinazowafanya wanawake wakimbie mahusiano na wanaume wenye tabia hizi:-

Kulazimishwa au kusukumwa kwenye maamuzi.
Wanawake hupenda mwanaume mwenye msimamo wake na mwenye kufanya maamuzi na kusaidia wenzie wanapohitahi msaada kutoka kwake pamoja nayeye mwenyewe bila shinikizo kutoka kwa yeyote. Usisukumwe sukumwe hovyo hata kama ikiwa na mama yako hili huonyesha udhaifu.

Ulevi wa kupindukia.
Sawa, Unywaji wa pombe haujawahi kupingwa ila endapo mwanaume ni mnywaji kupindukia kiasi anaweza akalala hata baa, akaazisha ugomvi au kuzima kabisa haipendezi. Hakuna kitu wanawake wanachukia kama mwanaume asiwejiweza anapokunywa pombe.

Matusi na lugha chafu.
Inawezekana wote kuna wakati huwa tunajikuta tunatumia maneno makali kama matusi na lugha chafu lakini lakini sasa inapofikia 60% ya maneno yanayotoka mdomoni mwako ni machafu, tena bila hata kuzingatia mahali ulipo, haipendezi tena si kwa mwanamke tu. Wanawake huwafurahia wanaume wanaojua nini aseme na akiseme wapi. Lugha chafu na matusi hayatakufikisha popote kwenye sekta hii ya mapenzi.

Kulalamika kuhusu mpenzi wako wa zamani.
Hamna anayejali kwamba mpenzi wako alikua mdanganyifu, alikuchuna au Malaya, kumlalamikia mwanamke wako wa sasa kuhusu mwanamke mwingine kunazidi kukupunguzia nafasi yaw ewe kuwa na mwanamke wa sasa kwa muda mrefu 1) atafikiri licha ya yote, bado unampenda 2) atafikiri hicho ndicho utakifanya kwa anayefuata baada yake kwa maana kwa sasa unalalamika bila upande wa pili kuwepo hivyo waweza kuwa unadanganya na ndicho utafanya na baada ya mahusiano haya.

Mwanaume king’anganizi mwenye kuhitaji zaidi na zaidi. 
Mwanaume analazimisha kupigiwa simu kila baada ya lisaa katika siku? Utadhani isipokua hivyo atafariki, na ukumbuke hapo hata hajawa Boyfriend bado, ndio kwanza anaongea na msichana. Jaribu kutafuta cha kufanya uwe busy kidogo hamna kitu kinakera kama mwanaume ambaye wanawake watafikiri hana kingine cha kufanya zaidi ya kufikiria mwanamke au mapenzi, mpe muda wa kukumiss ili akuze hisia zake kwako inavyotakiwa.

Mtu asiyejali familia wala rafiki zake.
Haitajalisha kabisa hata kama utamfanya yeye ajisikie kama Malkia, kama hujali familia yako hatavutiwa na wewe kwa imani kwamba utamfanyia hivyo nayeye pindi atakapokua mmoja kati ya wanafamilia kama mtafikia hatua ya kuoana. Jitahidi sana uwe na mahusiano mazuri na watu wanaokuzunguka, wanawake huliangalia hilo kwa wakati.

Uongo.
Kusema kweli, uongo kwa wanaume umekithiri, wengi wao huongea na uongo ili wapate wanachotaka vile inaaminika kwao bila longo longo maisha ya siku hizi huwezi kumpata mwanamke, la hasha, endapo mwanamke anagundua umemdanganya kitu, hata kama kilikua kidogo namna gani, imani na wewe inapotea. Hamna uongo mdogo na mkubwa, uongo ni uongo. Na hakuja jinsi ya kujielezea kwanini mtu ulidanganya wakati fulani na sasa unaamua kusema ukweli. Kuwa mkweli wakati wote.