Serikali ya Serbia yasisitiza kuendelea kutumia bidhaa za Huawei


Serikali ya Serbia imesema kuwa itaendelea kushirikiana na shirika la simu la China, Huawei licha ya Google kupiga marufuku Huawei kutumia huduma za Android.

Waziri mkuu wa Biashara, utalii na mawasiliano ya simu nchini Serbia, Tatjana Matic amesema kuwa Huawei ni moja wapo ya kampuni kubwa katika soko la Serbia, na shughuli zake si tishio kwa taifa hilo.

Utakumbuka Marekani ilisema kuwa Kampuni ya Huawei ni tishio kwa usalama wake kwa kuwa huenda kampuni hiyo inatumiwa na Uchina kufanyia serikali za nje na pia wananchi wake ujasusi.