TAKUKURU yawashikiria watu watatu, Diwani wa Ukonga ndani


Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU), inawashikilia watu watatu akiwamo Diwani wa Kata ya Ukonga (Chadema), Jumaa Mwipopo na Ofisa Mtendaji was kata hiyo, Rozalia Silumbe kwa tuhuma za kuomba Rushwa ya Sh.400,000 kwa mwananchi aliyekuwa anatuhumiwa kufanya uharibifu wa mazingira.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ilala, Christopher Myava amesema, watuhumiwa hao walikamatwa Mei 22, mwaka huu, saa 9 alasiri, Katika ofisi za Kata ya Ukonga.

Amesema watuhumiwa hao walishawishi na kuomba Rushwa ya Sh.400,000 na kupokea Sh.300,000 kutoka kwa mwananchi huyo.

“Watuhumiwa watafikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu tuhuma chini ya kifungu Cha 15 (1) (a)Cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11/2007,”amesema Myava.

Aidha Takukuru imewatahadhalisha wananchi kuacha kurubuniwa na matapeli na badala yake watoe taarifa mapema.