Uchebe kumuombea Mkewe Shilole


Mume wa mwanamuziki wa Bongo, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, Ashiraf Uchebe ameeleza kuwa yupo kwenye maombi kwa ajili ya kumuombea mkewe ili aendelee kubadilika na kuachana na mambo yasiyompendeza Mungu.

Uchebe alisema kuwa Shilole wa sasa sio wa zamani na kwa watu waliokuwa wakimjua lazima wanaona kuna mabadiliko makubwa.

“Hata hivyo sijachoka kwa sababu nampenda mke wangu huyu ambaye mimi naona ni zawadi kutoka kwa Mungu, bado nipo kwenye maombi ya kumuombea abadilike kabisa ili arejee kwa Mwenyezi Mungu mazima, Mwanzo nilidhani itakuwa kazi ngumu kumbadili lakini imekuwa rahisi sana na kila kukicha anabadilika,” alisema Uchebe.