Ujerumani yakubali kurejesha msalaba waliouchukua mwaka 1893


Ujerumani imekubali kurudisha msalaba uliouchukua nchini Namibia mwaka 1893, wakati ikitawala taifa hilo. Msalaba huo uliwekwa katika pwani ya Namibia na wachunguzi wa Ureno mwaka 1486. Namibia ilituma maombi ya kurejeshwa kwa msalaba huo miaka miwili iliyopita.