Vigezo vitakavyomfanya mwanamke aolewe mapema


Wapo wanawake ambao wao wanajua kila siku ni Ijumaa, yaani hawatambui kwamba kuna Jumamosi na Jumapili pia. Watu hawa ni wale wanaodhani maisha ni raha tupu na kwamba wanaoishi kwenye shida ni wajinga.Ukweli hauko hivyo, maisha yana changamoto nyingi sana. Kuna siku mambo yanaweza kuwa si mazuri lakini siku nyingine mambo yakawa supa. Mwanamke wa kuoa lazima ajue hivyo.

Vifuatavyo ndiyo vigezo vitakavyomfanya mwanamke aolewe mapema

Hana tamaa na pesa.
Katika maisha ya sasa mwanamke anayependa sana pesa ukikubali awe mkeo mtasumbuana sana. Kwa maana hiyo mwanamke ambaye utagundua hana tamaa ya pesa, kwamba ikiwepo, ikikosekana anabaki kuwa yeye, huyu ni ‘wife material’.

Hayupo tayari kukuona hauna amani.
Mwanamke ambaye unaona kabisa unapokuwa na matatizo anaumia, anahaha kuhakikisha anakurudisha kwenye hali ya kawaida, huyo anafaa kuwa mkeo

Hupenda watoto 
Utajuaje kama ana mapenzi na watoto? Iko hivi; katika uhusiano wenu ukiona ni mtu wa kupendapenda sana watoto wa marafiki zake, kuwanunulia zawadi, kuwashauri wenzake namna nzuri ya kuwalea watoto, hata akija kupata wa kwake itakuwa ni hivyohivyo.

Huwa anamuheshimu kila mtu
Msichana ambaye anaheshimu kila mtu, mdogo na mkubwa, anawapenda na kuwaheshimu ndugu, jamaa na marafiki zako, huyu ana sifa ya kuwa mkeo pia.

Anajishusha
Ogopa sana mwanamke ambaye anataka usawa. Anayekufaa ni yule anayejua yeye ni mke, na wewe ni mume. Anayetambua kuwa, mwanaume ndiye kiongozi wa familia.

Anakuongoza kwenye mambo mema.
Kama mpenzi wako ni wa kukutaka kila siku muende baa au mfanye madili hatari ili mpate pesa, huyu hana sifa ya kuwa mkeo. Mke ni yule ambaye atakuongoza kwenye kutenda mema na kuacha mabaya.

Kwa mfano kama unakunywa pombe atakushauri uache, kama siyo mtu wa ibada, atakushawishi umjue Mungu wako na mambo mengine kama hayo.

Anajua maisha na mapenzi kwa ujumla.
Mapenzi yanachukua sehemu kubwa ya maisha ya binadamu. Kwa maana hiyo mwanamke anayekufaa wewe ni yule ambaye anayajua mapenzi vilivyo lakini pia anajua maisha.

Kama yeye ni mtaalam wa majamboz tu lakini linapokuja suala la mambo ya kimaendeleo hayumo, huyo hafai. Pia akiwa yeye ni mtu wa mambo ya kimaendeleo tu lakini linapokuja suala la mapenzi ni sifuri, pia hakufai.