Wakulima kusajiliwa na kupewa vitambulisho


Akizungumza bungeni wakati wa kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara ya Kilimo, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imeamua kuanza kusajili wakulima wote nchini na kuwapa vitambulisho ikilenga kutambua walipo, mazao wanayolima na ukubwa wa mashamba yao

Waziri Hasunga ameeleza kuwa zoezi hilo linafanyika kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili kuwa na kanzidata ya uhakika ya kila zao baadaye kuwa na kanzidata moja iliyounganishwa kwa mazao yote.
Ameeleza kuwa hadi kufikia mwezi Machi 2019 jumla ya wakulima 1,464,827 wametambuliwa na kusajiliwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Kilimo ameeleza kuwa kwa takwimu za mwaka 2017 sekta ya kilimo ilitoa ajira kwa watanzania kwa asilimia 65.5 "Katika mwaka 2017, sekta ya kilimo ilitoa ajira kwa Watanzania kwa 65. ikichangia asilimia 28.7 ya pato la taifa ambapo sekta ndogo ya mazao ilichangia asilimia 65 ya malighafi za viwanda" Alieleza Waziri Hasunga