WHO yazindua mpango wa dunia kukabilia na kung'atwa na nyoka


Shirika la afya duniani WHO, hii leo limezindua mkakati mpya unaolenga kupunguza vifo na majeraha yanayotokana na kung'atwa na nyoka, likionya kuwa ukosefu wa dawa za kuuwa sumu unaweza kusababisha dharura ya kiafya.

 Kila mwaka, karibu watu milioni tatu hung'atwa na nyoka wenye sumu, na karibu watu kati ya elfu 81 na laki moja na 38 elfu hufariki dunia. Manusura wengine 400,000 hukumbwa na ulemavu wa kudumu na madhara mengine, kwa mujibu wa takwimu za WHO.

Katika ripoti yake mpya, shirika hilo la afya la dunia limeihimiza jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua kushughulikia tatizo hilo, ambalo linasema limepuuzwa kwa muda mrefu.