Yanga SC watuma salamu kwa wapinzani wao


Kocha Mkuu wa Yanga SC, Mwinyi Zahera ametamba na kueleza kwa sasa kikosi chake hakina huruma na timu yoyote itakayokutana nayo.

Leo Yanga SC watacheza na Ruvu Shooting FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Soka (TPL) utakaochezwa kwenye dimba la uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

"Tumejiandaa na mechi kama vile tunavyojiandaa katika mechi zingine, niseme tu hatuna huruma na
timu yoyote iliyoko mbele yetu, tunahitaji kupata ushindi na hatuna jambo jingine," amesema Zahera.

Kwa sasa Yanga SC wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi hiyo wakiwa wamejikusanyia pointi 80 katika michezo 35 waliyocheza hadi kufikia sasa, huku Simba SC wakiongoza kwa pointi 82.