Breaking News: Ajib, Mkude na Kapombe watemwa Taifa Stars


Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars inategemewa kusafiri leo kuelekea Misri ambako itaweka kambi kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Afcon.
.
.
Stars inasafiri na nyota 32 huku Nyota 7 wakiachwa. Nyota walioachwa ni Jonas Mkude, Ibrahim Ajib, Ayoub Lyanga, Ally, Khamis, Kennedy Wilson na Shomari Kapombe.
.
.
Kocha Amunike amesema kigezo kilichotumika kuwaacha nyota hao ni perfomance yao mazoezini na nidhamu huku akisisitiza anajua watu wanamatamanio yao juu ya wachezaji fulani lakin nidhamu na utimamu wa viwango vyao ktk mazoezi ni kipaumbele kikubwa mbali ya Kapombe ambaye bado hajawa fiti.
.
.
Aidha Amunike amesema amewajumuisha makinda Kelvin John na Boniphace ili kuwapa uzoefu zaidi akitambua umuhimu wa kuimarisha vijana kwa soka la baadae.