https://monetag.com/?ref_id=TTIb BREAKING: Wema Sepetu atupwa jela | Muungwana BLOG

BREAKING: Wema Sepetu atupwa jela


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuamuru msanii wa filamu nchini Wema Sepetu kwenda jela siku kuanzia leo hadi June 24 mwaka huu wakati akisubiria uamuzi wa mahakama wa kumfutia  dhamana.

Wema Sepetu anayekabiliwa na shtaka moja la kuchapisha video ya ngono na kusambaza katika mtandao wa kijamii wa Instagram.

Jumanne Juni 11, 2019 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilietoka hati ya kumkamata mlimbwende huyo wa Tanzania mwaka 2006, baada ya kukiuka masharti ya dhamana.