DC Ndejembi aahidi kumaliza tatizo la Maji Kongwa


Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Deo Ndejembi amefanya ziara ndani ya wilaya hiyo ambapo ametembelea mradi wa Maji wa Makawa wenye thamani ya Milioni 590.


Katika ziara hiyo DC Ndejembi amemuagiza mkandarasi wa mradi huo kuhakikisha anamalizia ujenzi huo ndani ya miezi mitatu kama ilivyokua imepangwa ili kumaliza tatizo la maji kwa wananchi.

"Tumetembelea pia mradi wa Matongoro wenye thamani ya Milioni 710, na tayari tumeanza kutoa huduma tuliyokua tumeikusudia kwa wananchi wetu. Pia nimefika  katika kijiji cha Mtanana ambapo kuna mradi wa maji unaoendeshwa na Solar. Lengo letu ni kuhakikisha tunamaliza tatizo la maji ndani ya Wilaya yetu," amesema DC Ndejembi.