Fahamu tatizo la mgongo wazi kiundani zaidi



Uti wa mgongo ulio wazi( Spinal bifida) ni hali ambayo mtoto anazaliwa nayo huku uti wa mgongo (mishipa ya fahamu mkubwa unaotoka kwenye ubongo) ukiwa wazi kutokana na mifupa (vipingili vya uti wa mgongo) kutokufunga vizuri.

Mgongo wazi(spinal bifida) inaweza pata watoto 3 kati ya watoto 10000 wanaozaliwa.

Uti wa mgongo hutengenezwa mara tu baada ya mimba kutungwa, ikiwa kuna kasoro katika utengenezaji wa uti huu basi sehemu fulani ya uti wa mgongo itabaki bila kuzibwa.

Visababishi 
Kuna sababu mbalimbali zinapelekea uti wa mgongo kutoziba, ambazo zinaweza zuhilika, nazo ni Upungufu wa folic acid(vit B9) na vitamin B12 katika kipindi cha ujauzito, katika kipindi cha miezi ya awali.

Mama mjamzito kupiga X-ray, mattumizi ya dawa za kifafa katika kipindi cha ujauzito .

Pamoja na maambukizi ya baadhi ya virusi kwa mama mjamzito.

Aina
Zipo aina mbiliza tatizo la tundu katika mgongo ama mgongo wazi

Aina ya kwanza ni occulta ambapo huwa na aina mbili pia, aina ya kwanza ni ile ambapo panakuwa na vinyweleo tu vinavyoonekana nyuma chini ya mgongo bila kuwa na dalili zozote zile, ama kunaweza kujitokeza kwa kuta zinazofunika mishipa ya fahamu tu.

Aina ya pili ni ni cystica ambapo panakuwa na vifuko vinavyofunika mishipa ya fahamu pamoja na mishipa ya kuchomoza katika tundu la mgongoni.

Aina hii ni mbaya zaidi kwani linaweza kusababisha mtoto asitembee ama asiweze kuzuia haja kubwa na ndogo.

Dalili
Dalili huwa kama zifuatazo
Kuwa na uvimbe nyuma chini ya mgongo.

Kuwa na vinyweleo sehemu za chini za mgongo bila kuwa na tatizo la mishipa ya fahamu
Kushindwa kutembea ama kukosa hisia katika miguu

Mtoto anaweza kushindwa kuzuia haja kubwa ama ndogo endapo mishipa yote ya fahamu imepita katika tundu hilo.

Na dalili zingine zinazoambatana kuharibika kwa mishipa.

Matibabu
Upasuaji
Upasuaji ni tiba pekee ya uti wa mgongo ulio wazi(spinal bifida) inayofanywa na madaktari bingwa wa upasuaji wa mishipa ya fahamu(neurosurgeons) wanachofanya ni kuziba lile tundu lililowazi.

Dawa na viinirishe 
Wanawake wengi walio katika kipindi cha kuzaa na wajawazito hawatumii vyakula vyenye vitamin B na folic acid inavyopaswa, vyakula hivyo ni matunda,mboga za majani, mbaazi na choroko.

Mwanamke mjamzito akipata lishe yenye virutubisho hivyo pamoja na kunywa vidonge vya folic acid, kwa asilimia 30% inaweza kupunguza hatarishi ya kupata watoto wenye uti wa mgongo ulio wazi.

Pia kwa wanawake wajawazito katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo, wanashauriwa kutokupiga X-ray.Inawezekana mwanamke akawa hatambui kama ni mjamzito,kipimo cha mkojo cha ujauzito(UPT-urinary pregnancy test) kifanyike kwa haraka kama mwanamke haelewi vizuri mzunguko wake wa hedhi kabla hajapiga X-ray ikiwa ana tatizo lingine la kiafya,

Mwanamke mwenye kifafa akiwa mjamzoto pia yupo kwenye matibabu, awahi haraka kwa daktari kushauriana ni nini zaidi cha kufanya ili kumsaidia.

Wanawake wajawazito wanashauriwa kuhudhulia kliniki mapema zaidi ili wapate elimu ya lishe na kuweza kuanza mapema kutumia folic acid kama kinga ya Mgongo wazi.

Kumbuka kwamba
Jamii inapaswa kujua kuwa Mgongo wazi(Spinal bifida) haitokani na mambo ya kishirikina bali ni hali ambayo inaweza kuzuilika. Mzazi yeyote mwenye mtoto mwenye Mgongo wazi anashauriwa ampeleke mtoto wake hospitali ili apate maelekezo ni wapi mtoto anaweza kupata matibabu ya upasuaji.)