Habari Picha: Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar akikagua ujenzi wa mitaro ya Maji ya mvua



Na Thabit Himidu, Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa Mtaro mkuu wa kupitisha maji ya mvua katika eneo la Kwa Abass Hussein hadi kinazini Mjini Magharib Unguja.

Lengo la ziara hiyo ni kuangalia athari ambazo zilizojitokeza wakati wa ujenzi wa mtaro huo.

Katika ziara hiyo makamu wa Rais aliambatana na viongozi mbalimbali wa mkoa na wa wilaya.