Hii ndio idadi ya wachezaji wanaotakiwa kusajiliwa Coastal Union

Kocha wa timu ya Coastal Union, Juma Mgunda amesema kuwa kwa sasa kikosi chake kinahitaji kusajili wachezaji sita ambao wataongeza nguvu ndani ya kikosi hicho.

Mgunda amesema kuwa ushindani msimu ujao utakuwa mkubwa tofauti na mwanzo hivyo ni lazima awe na kikosi makini kitakacholeta ushindani.

"Mpaka sasa bado mchakato wa usajili haujaanza ila hesabu ambazo zipo ni kuona kwamba tunasajili wachezaji sita ambao watakuja kuongeza nguvu pale ambapo kulikuwa na mapungufu kidogo msimu uliopita.

"Vijana wangu hawakuwa wazembe, wamepambana kufa na kupona ndio maaana tumebeki ndani ya ligi, msimu ujao ushindani utakuwa mgumu nasi tunapaswa tulete ushindani," amesema Mgunda.

Coastal Union kwa msimu wa 2018/19 inashikilia rekodi ya timu iliyofungwa mabao mengi baada ya kukubali kufungwa mabao 8-1 na Simba uwanja wa Uhuru.