Loading...

6/14/2019

Kampuni 600 zamtumia Trump barua

Zaidi ya makampuni 600 ya Kimarekani hapo jana yamemuandikia barua ya kumhimiza Rais wa Marekani Donald Trump kutafuta suluhisho la mgogoro wa kibiashara na China.

Barua hiyo imesema ushuru dhidi ya China unaumiza biashara ya Marekani pamoja na wateja.

Ni barua ya hivi karibuni miongoni mwa nyingi alizotumiwa Trump na kampeni ya kitaifa inayopinga ushuru inayojulikana kama "Ushuru unaumiza nchi" na kuungwa mkono na zaidi ya makundi 150 ya kibiashara yanayowakilisha sekta za kilimo, viwanda, biashara za rejareja pamoja na makampuni ya kiteknolojia.

Ni barua muhimu katika wakati ambapo mvutano wa kibiashara kati ya China na Marekani unazidi kuongezeka na kabla ya mkutano unaotarajiwa kati Trump na Rais wa China Xi Jinping wakati wa mkutano wa kilele wa kundi la mataifa 20 yaliyostawi kiviwanda ulimwenguni utakaofanyika mjini Osaka, Japan kuanzia Juni 28 hadi 29.
Loading...