Karibuni sana hapa ni nyumbani kwenu - Rais Magufuli


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kuwakaribisha wafanya biashara watano kutoka kila Wilaya amewakaribisha Ikulu na kuwaambia kuwa hapo ni nyumbani kwao.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo, wakati akiwakaribisha wafanyabiashara hao ili kujadili nao mambo mbalimbali.

Hata hivyo, Rais Magufuli amewashukuru wafanyabiashara hao kwa kufika kwa wingi japo kuwa ametoa mualiko huo kwa muda mfupi.

Wajumbe wote walitakiwa kuwasili katika ukumbi wa Kikwete kuanzia saa 2:00 hadi saa 2:30 asubuhi leo.