Kiungo wa Real Madrid kujiunga Atletico Madrid

Kiungo wa klabu ya Real Madrid, Marcos Lorente amekubali kujiunga kwa wapinzani wao Atletico Madrid.

Lorente atasaini mkataba wa miaka mitano na klabu hiyo kutegemea na vipimo vya afya.

Kiungo huyo mwenye miaka 24 ambaye amecheza mara 16 akiwa Real Madrid msimu uliopita, inasemekana dau lake la kwenda Atletico Madrid ni £35m.