Mabwana harusi milioni 115 wameozeshwa wakiwa bado watoto

Fuko la Umoja wa mataifa la msaada kwa watoto (UNICEF) limearifu kwamba duniani kuna watoto wa kiume milioni 115 waliozwa katika umri mdogo.

Kwa mara ya kwanza UNICEF imeandaa ripoti kuhusiana na mabwana harusi watoto baada ya kukusanya taarifa kutoka katika nchi 82. Kwa mujibu wa ripoti hio duniani kuna watoto wa kiume milioni 115 walioozwa katika umri mdogo, miongoni mwa watoto hao 1 ya 5 wameozeshwa wakiwa na umri chini ya miaka 15.

Jamuhuri ya Afrika ya kati inaongoza kwa kuwa na asilimia 28 ya mbawana harusi watoto, ikifutiwa na Nikaragua ikiwa na asilimia 19, Madascar imeshika nafasi ya 3 ikiwa na asilimia 13.