Mapigano bado yaendelea Libya

Vita kali inaendelea kuzunguka eneo la uwanja wa ndege wa Tripoli ikihusisha majeshi ya serikali ya makubaliano ya kitaifa Libya na majeshi ya Jenerali Haftar.

Ndege za kivita za majeshi ya Haftar zilipiga maeneo mbalimbali ya majeshi ya serikali yaliyopo Tripoli na Tacure.

Meya wa mji waTacure aliwaambia wanahabari kwamba kutokana na mashambulizi hayo yaliyofanywa na vikosi vya Jenerali Haftar, baadhi ya raia walijeruhiwa.

Kiongozi wa kijeshi anayeongoza mashariki ya Libya, jenerali Khalifa Haftar alitoa amri ya kushambulia ili kuikamata Tripoli mnamo April 4, Kutokana na amri hiyo walianzisha oparesheni dhidi ya majeshi ya serikali yaliyopo katika mji wa Tripoli.