Baraza la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limepiga marufuku matumizi ya vifungashio vinavyotumika kuwa vibebesheo vya bidhaa mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt Samuel Gwamaka amesema vifungashio vimeingia kwa kasi kutumika kwa ajili ya kubebea bidhaa mbalimbali ambapo hakuna tofauti na mifuko ya plastiki ya Rambo na Mifuko laini Soft (Rambo).
Amesema kuwa NEMC inaingia mtaani kwa nchi nzima kuangalia mifuko hiyo na atakayekutwa na mifuko hiyo ashike faini ya sh.30,000 na kuendelea.
"Serikali imepiga marufuku mifuko ya plastiki hivyo hakuna njia mbadala ya kutumia mifuko hiyo plastiki kwa kudai mifuko ya vifungashio imeruhusiwa"amesema Gwamaka.
Gwamaka amesema watu wakiingia mtaani mifuko yoyote ile kwani mifuko mbadala ipo lakini mingine ina ghafi ya plastiki itaondolewa katika soko. Aidha amesema kuwa wananchi watoe ushirikiano ikiwa ni kuacha kutumia mifuko ya plastiki wanayodai vifungashio.