Loading...

6/13/2019

Nilipokuwa Waziri niliwahi kuteua mtu wa darasa la 7 - Rais Magufuli


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema alipokuwa Waziri wa Ujenzi aliwahi kuteua mtu wa darasa la saba kuwa meneja wa Tamesa mkoa wa Kagera..

Rais Magufuli ameyasema hayo leo, Ikulu jijini Dar Es Salaam alipokutana na Wabunifu wa mitambo midogo ya kufua umeme kwa kutumia maji ya mito ambapo ameseam kuwa alifanya hivyo baada ya kuona utendaji kazi wake ni mzuri.

"Mimi nilipokuwa Waziri wa Ujenzi nilishawahi kumuweka darasa la saba, akawa Meneja wa Mkoa wa Kagera kwenye Tamesa kwasababu alikuwa anacorrect vizuri revenue kuliko wenye degree sasa nielezee plan zako ili nisije nikamteua mmoja kuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji Tanzania ," amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli amesema kuwa huyo wa la saba alikuwa na utendaji mzuri kuliko hata wale wenye degree.

Loading...