https://monetag.com/?ref_id=TTIb Prof. Kabudi awapa neno Waandishi wa habari | Muungwana BLOG

Prof. Kabudi awapa neno Waandishi wa habari


Wakati Tanzania inajiandaa kupokea Mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) mapema Agosti, vyombo vya habari vimekumbushwa umuhimu wa kuzibaini fursa za uwekezaji ili kuzitangaza kwa nchi zitakazoshiriki ili wawekezaji watakaofika nchini kuweza kuvutiwa kuwekeza nchini,

Mbali na mkutano huo wa SADC  utakaofanyika jijini Dar es Salaam Agost 17 -18. 2019 baada ya karibu miongo miwili, katika viwanja vya Mlimani City yatafanyika maonesho ya Wiki ya Viwanda Julai yatakayoanza  22-26,2019, ikiwa ni fursa ya kutambua nafasi ya viwanda katika nchi za SADC.

Akiongea na wamiliki wa vyombo vya habari na wahiriri, jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, amekumbusha wanahabari kutangaza dhima ya serikali ya kujenga viwanda, nafursa za kuwekeza katika kilimo, utalii na maeneo mengine.

Waziri amesema,”nafasi  yenu waandishi sio kuripoti tuma tukio katika siku za mkutano wa SADC, ni muhimu kushiriki katika hatua ya kuandaa, kushiriki mkutanoni na hata baada ya mkutano kushiriki tathmini ya hatua zote za vikao mbalimbali vya SADC na Mkutano Mkuu” amesisitiza

Pamoja na ajenda ya uwekezaji, Waziri huyo ambaye kiutumishi alianza na taaluma ya habari amewakumbusha waandishi juhudi za Tanzania baada ya Uhuru 1961 za mwalimu Nyerere alivyopigania Bara la Afrika, huku akizitaja nchi za Angola, Msumbiji, Afrika Kusini, Kenya, Rwanda na Burundi zilivyosaidiwa na Tanzania katika harakati zao zakujikomboa kutoka utawala wa wakoloni.

“Vijana wengi wa kizazi cha sasa hawajui heshima kubwa inayostahili Tanzania kutokana na mchango wake kwa  nchi zinazotuzunguka … wanatakiwakujua, vyombo vya habari havielezei historia ya nchiyetu,” Waziri Kabudi amesema huku akiwasisitiza waandishi wakongwe kuwashirikisha waandishi vijana kujua yaliyofanywa na taifa lao baada ya Uhuru kukomboa nchi za kusini mwa Tanzania.

Nchi 16 za SADC zenye watuzaidi ya milioni 450 zina nafasi kubwa kunufaika na Tanzania kupata mali ghafi ya viwanda kutokana na nchi kuwa na nafasi kubwa ya ardhi ya rutuba ya kuweza kulima aina nyingi za mazao, pia ardhi yake kuwa na hifadhi ya maji mengi kwa kilimo na hifadhi za wanyama.

Waziri amesisitiza kwa  jamii ya watanzania kuona umuhimu wa mkutano huo, ambapo unakuja Tanzania tokea mwaka 2003, wakati nafasi ya Uenyekiti ulikuwa kwa Rais wa Tanzania (wakati huo), Benjamin Mkapa, kwa sasaRais wa NamibiandiyeMwenyekiti, baada ya kupokea toka Afrika Kusini na Makamu wake ni Rais wa Tanzania, Dkt John Magufuli atakabidhiwa nafasi ya uenyekiti Agost 18, 2019.