Raia wa Sudan waandamana mjini Istanbul

Raia wa Sudan mjini Istanbul wamekusanyika kupinga mauaji yanayofanywa na vikosi vya jeshi dhidi ya wananchi wanaofanya maandamano ya amani nchini Sudan.

Maandamano mjini Istanbul yamefanywa huku raia hao wakiwa wamebeba bendera za Sudan na Uturuki wakitaka haki,uhuru na amani.

Utawala wa miaka 30 wa Omar al Bashir uliondolewa na maandamano ya wananchi wa Sudan na baadaye uongozi kuchukuliwa na jeshi la nchi hiyo.

Raia nchini Sudan wamekuwa wakiandamana kwa amani wakitaka utawala kwa kiraia nchini humo na sio jeshi.

Kwa mujibu wa habari,vikosi vya jeshi la nchi hiyo vimekuwa vikiua wananchi wasio na hatia na kurusha miili yao katika mto Nile ili kufuta ushahidi.

Ni idadi kubwa ya wanawake wamebakwa huku raia wengine wakiwa wamejeruhiwa vibaya na wanajeshi hao.

Taarifa pia imedai kuundwa kwa baraza la uchunguzi wa kujitegemea kwa mashtaka ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Sudan, ufunguzi wa haraka wa huduma ya mtandao, ambayo ilikuwa imekatwa kwa wiki mbili nchini kote, na kuwekwa mara moja kwa utawala wa kiraia.

Maandamano yalisitishwa mjini Istanbul baada ya tangazo hilo kutolewa.