Loading...

6/13/2019

Rais Magufuli awapa Milioni 5 wabunifu wa mitambo midogo ya kufua umeme


Rais Magufuli amekutana na Wabunifu wa mitambo midogo ya kufua umeme kwa kutumia maji ya mito kutoka  Njombe, Mzee Jairos Ngailo na John Mwafute maarufu kama Pwagu.


Rais amekutana na wabunifu hao Ikulu jijini Dar Es Salaam amesema kuwa hizo hela alizowapa wataenda kula kwaajili ya kuhangaika kwao.


"Na mimi angalau niwachangie wote Milioni 5 wote wawili na nyinyi mtaenda kula kwa kuhangaika kwenu nina Milioni 5 hapa mtagawana ," amesema Rais Magufuli.

Haya ni baadhi ya maswali waliyokuwa wakiulizwa wabunifu hao na Rais Magufuli;

Rais Magufuli : Hesabu wewe mzee Pwagu

Mzee Pwagu: Siwezi kuhesababu macho hayaoni vizuri

Rais Magufuli :kwa sababu ya kupigwa na mitambo ya umeme

Mzee Pwagu: Eeeh!

Rais Magufuli: hawa TANESCO wala hawajali?

Mzee Pwagu: Aaah amna

Rais Magufuli: Hata watu wa Wizara ya Maji wameshawahi kuja kukuona?

Mzee Pwagu: Hata siku moja

Rais Magufuli: Kwahiyo hii Pampu ulitengeneza mwenyewe?


Mzee Pwagu: Ndio

Mzee Pwagu: Mh. Rais Wajerumani ndio wanaotusaidia ila Watanzania Hapana

Rais Magufuli :Mzee usikate tamaa Mungu yupo


Loading...