Loading...

6/12/2019

Rais Magufuli kuwa Mwenyekiti wa SADC


Rais John Magufuli anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa SADC kuanzia Agosti 17 mwaka huu hadi Agosti 17, 2020.

Taarifa hiyo imetolewa leo, Jumatano na Waziri wa Mambo ya Nje, Profesa Palamagamba Kabudi alipokutana na watendaji wakuu wa vyombo vya habari kujadiliana kuhusu maandalizi ya Mkutano huo Mkuu wa SADC utakaofanyika jijini Dar es Salaam ikiwa ni miaka 16 tangu ufanyike nchini mwaka 2003.

Jumla ya wakuu wa nchi 16 kutoka Angola, Botswana, DR Congo, Lesotho, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Shelisheli, Afrika Kusini, Swaziland, Zambia na Zimbabwe wanatarajiwa kushiriki mkutano huo.
Loading...