Loading...

6/14/2019

Real Madrid yamsajili Messi wa Japan

Real Madrid imemsajili mshambuliaji wa Japan Takefusa Kubo, ambapo klabu hiyo ya Hispania inasema kinda huyo mwenye miaka 18 anatarajiwa kuwa bora zaidi na pia anachukuliwa kama Messi wa Japan.

Kubo, 18, anatajia kusaini mkataba wa miaka mitano na ataingizwa kwenye timu B ya Real Madrid inayoshiriki ligi daraja la tatu Hispania.
Loading...