Loading...

6/17/2019

TANZIA: Mwanafunzi wa Chuo Kikuu afariki dunia kwa kushambuliwa na vibaka


Mwanafunzi wa Stashahada ya Maabara katika Chuo Kukuu cha Kampala tawi la Tanzania, Anifa Mgaya amefariki kwa kile kinachoelezwa kuwa amevamiwa na vibaka.

Taarifa zinadai kabla ya umauti kumfika Anifa (pichani juu) alichomwa visu viwili na watu wasiojulikana majira ya saa mbili usiku jirani na geti la kuingia Chuo kikuu cha Kampala.

Marehemu alianguka chini na kuomba msaada kutoka kwa wasamaria wema ambao baadhi walikuwepo eneo la tukio, lakini hakuna aliyejitolea msaada wakidai watapata kesi isiyowahusu.

Baadae wakajitokeza baadhi ya wanafunzi kumpatia msaada wa haraka kumfikisha hospitali ambapo hata hivyo tayari mauti yalishamfika binti huyo.

Loading...